Search This Blog
Saturday, August 24, 2019
Kondomu Milioni 30 zaagizwa kutoka nje
Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) imeagiza kondom milioni 30 kutoka nje ya nchi kupitia Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na kuzisambaza nchini.
Taarifa hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk Leonard Maboko baada ya kutembelea mradi wa Timiza Malengo unaojihusisha na kinga dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na athari za Ukimwi kwa wasichana Balehe na Wanawake Vijana wilayani Mpwapwa.
Dk Maboko amesema MSD imeziingiza kondomu hizo nchini na kuagiza zisambazwe katika maduka yao yaliyopo kwenye kanda ili kuhakikisha zinafika katika hospitali mbalimbali.
Alisema kutoka katika maduka ya kanda zitasambazwa kwenye ngazi ya hospitali za mikoa, wilaya na hata katika zahanati zilizoenea nchi nzima.
Dk Maboko amesema ni kweli kulikuwa na upungufu wa kondomu zinazogawiwa bure katika kipindi cha miezi michache iliyopita, lakini sasa kondomu zipo.
Alisema kinachotakiwa ni MSD kusambaza kwa haraka kondomu na kufikisha katika maeneo mbalimbali nchini ili kuwafikia wananchi katika zahanati na vituo vya afya vilivyo karibu nao.
Alisema atawasiliana na wizara kuhakikisha zinasambaa zaidi ili kutoka maduka ya MSD ya kanda na kuhakikisha zinafika katika zahanati mbalimbali nchini ambazo zipo katika maeneo ya vijijini.
Dk Maboko amesema pia tume hiyo inaendelea na mazungumzo na Shirika la kimataifaf linaloitwa Global Fund ili kuhakikisha zinapatikana kondomu nyingine zaidi ya milioni sita ili kumaliza uhaba nchini.
Amesema katika kuthibitisha kwamba hakuna tatizo hilo, barua ziliandikwa katika halmashauri na wilaya mbalimbali kueleza kwamba hakuna tatizo la kondomu baada ya kwamba zimeagizwa kupitia MSD.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment