Search This Blog
Friday, August 2, 2019
China Yaahadi Kulipa Kisasi Dhidi ya Ushuru wa Marekani
China imesema inajitayarisha kuchukua hatua za kulipa kisasi iwapo rais Donald Trump wa Marekani ataendelea na mipango yake ya kuongeza ushuru kwa bidhaa za China zenye thamani ya dola bilioni 300 mwezi Septemba.
Nyongeza hiyo ya ushuru wa asilimia 10 ambayo huenda itazilenga bidhaa za elektroniki na mavazi, itamaanisha kuwa karibu bidhaa zote za China zinapelekwa Marekani zitalipiwa kodi.
Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa China, Hua Chunying, amesema pindi Marekani itaendelea na mipango yake ya kuongeza ushuru, China itajibu kwa kuchukua hatua sawa kulinda maslahi yake.
Ingawa Chunying hakueleza hatua ambazo nchi hiyo itachukua, afisa huyo amesisitiza kuwa China haitokubali shinikizo, vitisho na ulaghai kutoka Marekani.
Rais Trump ametishia mara kadhaa kuendelea kuongeza ushuru kwa bidhaa za China ikiwa rais Xi Jinping hatoharakisha mipango ya kufikia makubaliano ya kibiashara
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment