Search This Blog
Sunday, August 4, 2019
Alichokisema Dkt. Bashiru kuhusu wanaogawa fedha CCM
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally amesema chama hicho hakitakuwa na msalie mtume kwa mtu yeyote atakayetumia jukwaa la uchaguzi na fedha katika kuwagawa Watanzania.
Dk. Bashiru ameyasema hayo jijini Mwanza wakati alipozungumza katika Kongamano la Vyuo Vikuu la wanachama wa CCM kutoka vyuo hivyo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Gandhi.
Alisema wapo watu kwa sasa ambao wameanza kuzunguka nchi nzima wengi wao wakiwa na mambo ya kupotosha na kutokubali juhudi ambazo zimekuwa zikifanywa na Serikali ya CCM chini ya uongozi wa Rais John Magufuli wa kuwaletea wananchi maendeleo.
"Tayari wameishaanza kujipitisha, niseme tu wakati wa uchaguzi ni wakati wa kuwachagua viongozi bora,"alisema.
Aidha, aliongeza kuwa CCM haitamvumilia mtu yeyote atakayeonesha nia ya kuvuruga Muungano, Mapinduzi ya Zanzibar, Mwenge wa Uhuru sanjari na kuibeza lugha ya Taifa ya Kiswahili, na kwamba watu wa aina hiyo watakuwa ni wasaliti wa juhudi zinazofanywa na serikali za kuwaletea wananchi maendeleo.
Dk Bashiru ambaye ni Mlezi wa Chama wa Mkoa wa Mwanza, alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na watendaji wake kwa kazi kubwa wanayofanya, ikiwemo jinsi ambavyo mkuu huyo wa mkoa alifanya kazi kubwa ya uokoaji wa watu na mali zao wakati wa kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe mwaka jana.
"Wale waliokuwa wanadhani Mongella atagombea ubunge katika Jimbo la Ilemela nafasi hiyo haipo kwa sasa, ataendelea kufanya kazi," alisema Dk Bashiru.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment