Search This Blog
Saturday, July 20, 2019
Takukuru yataka wajumbe ardhi wapewe elimu kupunguza malalamiko
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Ruvuma, Yustina Chagaka ameitaka idara inayoshughulika na masuala ya ardhi mkoani humo kutoa elimu ya mara kwa mara kwa wajumbe waliopo katika mabaraza ya ardhi ili kupunguza malalamiko.
Wito huo umetolewa na mkuu huyo ofisini kwake, wakati akitoa taarifa ya utekelezaji ya robo mwaka kwa waandishi wa habari.
Alisema idara ya ardhi, inaongoza kulalamikiwa na wananchi mbalimbali na kumekuwapo viashiria vya mianya ya rushwa.
Alisema utendaji kazi wa robo ya mwaka, kumekuwapo na malalamiko mengi yanatoka sekta ya ardhi ambayo hadi sasa yamefika 17.
Alisema migogoro inayoshughulikiwa na mabaraza ardhi ya vijiji na kata,wajumbe wake wengi wameteuliwa kushughulikia migogoro hiyo huku hawana elimu ya utambuzi kuhusu masuala ya ardhi.
Alisema baadhi ya wajumbe, wanatumia nafasi hiyo kujipatia vipato kwa walalamikaji kwa kuwaambia watoe gharama za kwenda maeneo ya migogoro ambako mwisho wa siku anayetoa kiasi kikubwa ndiye anayeonekana mwenyewe haki.
“Ofisi yangu imepata malalamiko mengi kutoka idara hii, tumejipanga kupambana nalo kisawasawa haiwezekani migogoro imekuwa mingi mno eneo hiuli,”alisema Chagaka.
Alisema idara zingine zinazolalamikiwa na idadi ya malalamiko katika mabano, ni elimu (10), halmashauri (7),Serikali za mitaa (5), polisi (5),vyama vya ushirika (4), mahakama (4), maji (3) na taasisi za fedha (2). Kuhusu miradi ya maji, alisema kwa asilimia kubwa imekuwa na matatizo kukamilika
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment