Search This Blog
Wednesday, July 3, 2019
Taarifa muhimu kutoka TCRA kuhusu Mawakala wanaosajili laini za simu
Wakati Mamlaka ya Mawasiliano Tanzaia (TCRA) inaendela na utekelezaji wa zoezi la usajili wa laini za simu kwa njia ya biometria, TCRA imebaini kuwa kuna watu wanaojihusisha na usajili wa Simu bila kuidhinishwa na watoa huduma za mawasiliano.
Kwa mujibu wa kifungu cha 92 na 97 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, 2010 na Kanuni ya 9,10, na 11 ya Kanuni za Usajili wa Laini za Simu (Sim Card Registration Regulations, 2018), TCRA inapenda kuutaarifu na kuukumbusha Umma kuwa:-
Ni marufuku kwa mtu yeyote kuuza, kusambaza au kusajili laini za simu bila kuwa na uthibitisho kuwa ameidhinishwa na mtoa huduma za mawasiliano kutoa huduma hizo;
Yeyote anayejihususha na uuzaji, usambazaji au usajili wa laini za simu anatakiwa kuwa na ofisi ya kutolea huduma hiyo ya usajili wa laini za simu; na Ni kosa la jinai kwa mtu yeyoye kuuza, kusambaza au kusajili laini za simu bila kuwa na ofisi na uthibitisho wa idhini ya mtoa huduma husika.
Umma unakumbushwa na kuonywa kuwa hatua zaidi zitachukuliwa, ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani pamoja na faini, kwa mtu yeyote atakaye bainika kuuza, kusambaza au kusajili laini za simu bila kufuata taratibu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment