Search This Blog
Wednesday, July 3, 2019
JKT yaomba taarifa hii kupuuzwa
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linapenda kukanusha taarifa zinazoendelea kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii, zinazoelezea kuhitajika kwa vijana wa JKT kundi la kujitolea Operesheni Kikwete na Operesheni Magufuli kukusanyika katika Kambi ya JKT Mgulani jijini Dar es Salaam tarehe 08 Julai 2019 kwa ajili ya usaili.
Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa yanazikanusha taarifa hizo za uzushi zenye lengo la kuwachanganya vijana wetu ambao wamehitimu mafunzo ya JKT na kurejea makwao.
Siku zote JKT imekuwa ikisisitiza kuwa vijana wanaojiunga na mafunzo ya JKT ni vyema wakatambua kuwa mafunzo hayo hayana uhusiano wa kupatiwa ajira kwenye vyombo vya ulinzi na usalama mara wamalizapo mkataba, bali mafunzo hayo yanawajengea uwezo wa kujuwa stadi za kazi na stadi za maisha.
Jeshi la Kujenga Taifa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wanafatilia kwa karibu kikundi kidogo chenye tabia ya kusambaza taarifa potofu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment