Search This Blog
Monday, July 1, 2019
Kamanda Mambosasa amjibu Zitto Kabwe
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema taarifa zilizotolewa na Zitto Kabwe kuhusu mahali alipo Raphael Ongangi raia wa Kenya anayedaiwa kutekwa Juni 24 ni taarifa za mitandaoni na wao hawafanyii kazi mambo ya mitandao.
Hata hivyo Jeshi la Polisi limewataka watu wenye taarifa kuhusu tukio la kutekwa kwa Bw. Ongangi, waziwasilishe ili ziweze kufanyiwa kazi.
Hapo jana Zitto Kabwe ameelezea simu yake ilivyodukuliwa akihusisha tukio hilo na lile la kudaiwa kutekwa kwa msaidizi wake, Raphel Ongangi raia wa Kenya.
Kutokana na hali hiyo, Zitto amewataka watekaji hao kumwachia huru kwani hana taarifa zake wanazozihitaji. Raia huyo wa Kenya anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana jijini Dar es Salaam, wakati akitoka shuleni kwa watoto wake kwenye kikao cha wazazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment