Search This Blog
Monday, July 15, 2019
Anapewa kibali cha kwenda kutibiwa India lakini anaumwa mafua - Rais Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemwagiza Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kufuatilia malipo yote ya Wagonjwa wanoenda kutibiwa nje ya nchi ili kubaini ubadilifu unaofanywa na baadhi ya watu wasiowaaminifu.
Rais Magufuli ameagiza hilo jana wakati akizindua miradi Saba ya huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Ziwa Bugando yenye thamani ya shilingi Bilion15, jambo litalosaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma bora kwa ukaribu pamoja na kuokoa kiasi cha fedha miongoni mwa wanaohitaji huduma.
"Na kwasababu Waziri wa Afya yupo hapa, akafuatilie malipo yote ambayo tunatakiwa kulipa, kule nje , akikuta kunamalipo yakulipa mtu ambae hakuwa mgonjwa aliyejihifadhi huko, akazilipe mwenyewe " alisema Rais Magufuli.
Rais Magufuli amesema kuwa baadhiya Watendaji waliona kupeleka Wagonjwa nje ya nchi kwaajili ya matibabu ni fursa yakujipatia kipato, jambo lililokuwa linapelekea hasara kubwa kwa nchi ya Tanzania kutokana na malipo kwa baadhiya watu wasiostaholi.
"Hata kupeleka kwa wagonjwa nje kwa Watanzania ilikuwa ni dili, ilikuwa ni fursa kwa Watendaji, wapo watu waliokuwa wanapewa vibali kwenda kutibiwa India lakini anaumwa mafua, ilikusudi apate safari na msindikizaji, bill zote zinaletwa kwa Serikali " alisema Rais Magufuli.
Dkt. Magufuli aliendelea kusema kuwa ni lazima tujenge nidhamu katika nchi, huku akisisitiza kuwa Serikali haijakataza kupeleka wagonjwa nje ya nchi, huku akisisitiza kuwa wagonjwa wanaostahili kupelekwa kwa matibabu nje ya nchi ni wale walioshindikana ndani ya nchi.
Aidha, Rais Magufuli ameagiza kuboresha uzalishaji wa oksijeni ili kuhakikisha zinazalishwa kwa wingi jambo litalosaidia kuokoa kiwango kikubwa cha mapato kinachopotea kwa kuagiza nje ya nchi, pia itasaidia kuongeza ajira kwa wananchi wa Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment