Search This Blog

Tuesday, June 11, 2019

Zitto Kabwe aishushia tuhuma nzito CCM kuhusu uchumi


Kamati Kuu ya chama cha ACT Wazalendo imetoa maazimio juu ya hali ya nchi baada ya kukaa kwa siku mbili katika kikao chake cha kawaida ambapo ilipitia hali ya Kisiasa na kiuchumi nchini pamoja na Bara la Afrika kwa ujumla.

Akiwasilisha maazimio hayo  mbele ya waandishi wa habari katika ofisi ndogo ya chama hicho Magomeni jijini Dar es Salaam, Kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe amesema moja ya maazimio waliyofikia ni kasi ya ukuaji wa uchumi kuporomoka kutokana na Serikali ya CCM ya awamu ya tano chini Rais John Magufuli kukata nishati ya kuendesha uchumi.

“Takwimu za benki Kuu ya Tanzania zinaonyesha mwaka unaoishia Machi 2018 urari wa biashara kati ya Tanzania na nchi nyingine duniani ulikuwa hasi kwa dola bilioni 2, Kwa mwezi unaoishia Machi 2019 urari wa biashara umetanuka kufikia hasi ya dola bilioni 2 sawa na ongezeko la dola milioni 500,” amesema.

Ameongeza kuwa Kupungua kwa Uwekezaji nchini (FDI) kunapekelea shughuli za Uchumi kutoongezeka, kutozalisha ajira rasmi za kutosha na kutoongeza mapato ya Serikali.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...