Search This Blog

Tuesday, June 11, 2019

RC Katavi atoa onyo kali kwa Wanasiasa


Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera amesema licha ya kutafsiriwa vibaya kwenye baadhi ya vyombo vya habari, hatasita kuchukua hatua kwa watu wote wanaofanya kampeni za kupita nyumba kwa nyumba kuwashawishi wananchi kwa lengo la kufanikisha mambo yao ya siasa.

Juma Homera ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali waliomtembelea ofisini kwake kwa lengo la kujua mikakati na mipango ya maendeleo ya mkoa huo katika kuwaletea maendeleo wananchi.

“Nawaonya wananchi hususani wanasiasa kuacha kufanya siasa za nyumba kwa Nyumba kwa sababu muda wa siasa hizo  bado na msajiri wa vyama vya siasa alishapiga marufuku mikutano hiyo kasoro ile ya ndani tu ,vinginevyo sheria itachukua mkondo wake.

Homera amesema marufuku hiyo ni kwa vyama vyote vya kisiasa nchini ikiwemo CCM na vyama vingine vyote vya siasa.

“Hii ni Juni,wanasiasa wakae wasubiri muda mwafaka ufike wafanye wanachokifanya na tena ni kwa mujibu wa sheria,si kiholelaholela,” amesema.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...