Search This Blog
Tuesday, June 25, 2019
Waziri Ummy asisitiza ubora wa bidhaa katika kiwanda cha dawa Simiyu
Bodi ya wakurugenzi wa kiwanda cha vifaa tiba cha Simiyu (SIMIYU MEDICAL PRODUCTS) wametakiwa kuzalisha bidhaa zenye viwango na kukidhi mahitaji ya ndani nan je ya nchi.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa bodi ya wakurugenzi wa kiwanda hicho uliofanyika leo jijini hapa.
Waziri Ummy amesema kuwa bidhaa zenye viwango itasaidia kuuza nje ya nchi na watanzania kuzitumia kwani lengo la serikali ya awamu ya tano ni ya kukuza uchumi wa viwanda
“Lakini mhakikishe maamuzi yeyote mtakayofanya mjiridhishe je ni kwa ajili ya maslahi ya Taifa na je yatatufikisha kule tunapotaka kufika,jiridhisheni katika kuhakikisha mnatumia fedha hizi chache tulizonazo katika kuleta matokeo ya haraka haya ndiyo ya kuyazingatia” alisema Waziri Ummy.
Aidha, Waziri Ummy aliitaka bodi hiyo kuhakikisha wanaongeza thamani ya mazao ya nchi kwa kuzalisha bidhaa nchini na kuondokana na uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi,kuongeza ajira na hata kuondokana na uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi.
Hata hivyo aliwataka wasiangalie bidhaa zinazotakana na pamba hivyo kwa baadae ni bora wakaangalia bidhaa zingine zinazohitajika ambazo zinanunuliwa kwa haraka sana kutoka MSD kwani bohari ya Dawa hivi sasa imepata mkataba wa kununua bidhaa za hospitali kwa niaba ya nchi kumi na sita za nchi ya SADC hivyo wahakikishe bidhaa zinazozalishwa zina viwango na ubora na uzalishaji unakidhi soko la ndani nan je ya Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment