Search This Blog

Tuesday, June 18, 2019

Wastaafu watakiwa kuzingatia mabadiliko ya maisha baada ya kustaafu


Watumishi wanaotarajia kustaafu wameaswa kuzingatia mabadiliko ya maisha kutoka katika utumishi wa umma kwenda katika mfumo wa maisha ya  kawaida na kujiepusha kufanya miradi ambayo hawana ujuzi wa kutosha.

 Akizungumza katika mafunzo kwa yakuwajengea uwezo watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajia kustaafu hivi karibuni ili wawe na mbinu za kuendana na mazingira hayo, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo anayeshughulikia (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko amesema kuwa Ofisi hiyo inatambua umuhimu wa wastaafu na faida za kujiandaa kustaafu.

“Kuna umuhimu mkubwa wa kutambua kuwa suala la kustaafu ni la kila mmoa wetu na ni muhimu kujiandaa vyema na maisha mapya ambayo kimsingi yatakuwa tofauti na haya ya utumishi wa umma mliyo nayo  kwa sasa” Alisisitiza Mwaluko.

Akifafanua amesema kuwa kila mtumishi wa umma lazima atambue kuwa ni mstaafu matarajiwa hivyo kujiandaa kwake ni jambo  muhimu.

Kwa upande wake, Muwezeshaji Kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma Magogoni Jijini Dar es Salaam, Bw. Peter Seme amesema kuwa watumishi hao wanaotarajia kustaafu watajifunza mambo mengi yakuwawzesha kuendelea na maisha yao kama kawaidia hata baada ya kustaafu.

Alitaja baadhi ya mada kuwa ni pamoja na utayari wa kupokea mabadiliko baada ya kustaafu, Stadi za kuongeza kipato, Mtindo wa maisha bora baada ya kustaafu, Namna ya kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza baada ya kustaafu.

Kwa upande wake mmoja wa watumishi hao,  Bw. Esamo Sawaki amesema kuwa  wanaipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuandaa mafunzo hayo kwa ajili ya kuwajengea uwezo watumishi wa Ofisi hiyo ili waweze kukabiliana na changamaoto zinazoweza kujitokeza baada ya kustaafu

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...