Search This Blog

Tuesday, June 18, 2019

Marta azidi kutisha Brazil, aweka rekodi hii ya dunia


Mchezaji bora wa mwaka wa dunia mara sita (6) Marta ameweka rekodi mpya kwenye fainali za kombe la dunia kwa kufikisha magoli 17 alipoifungia Brazil bao pekee dhidi ya Italy lililoipeleka hatua ya 16 bora (mtoano).

Mwanamama huyo mwenye miaka 33 alikwamisha bao kwa mkwaju wa penati na kuandika rekodi ya kuwa mfungaji wa muda wote wa fainali za kombe la dunia kwa wanawake na wanaume akiivunja rekodi ya striker wa zawani wa Ujerumani Miroslav Klose.

Wafungaji wa muda wote fainali za kombe la Dunia ni Marta 17, Klose 16, Ronaldo 15, Muller 14 na Prinz 14.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...