Search This Blog

Tuesday, June 11, 2019

Wanaowabaka watoto kuondolewa nguvu za kiume


Jimbo la Alabama nchini marekani limepitisha muswada wa sheria inayowalazimu baadhi ya watu waliopatikana na hatia ya kuwabaka watoto kupitia tiba ya kemikali itakayowaondolea uwezo wa nguvu za kiume.


Chini ya sheria hiyo, wale watakaopatikana na hatia ya kosa la kufanya tendo la ngono na watoto mwenye umri wa chini ya miaka 13 watalazimika kuanza kupata dawa za kuwapunguzia uwezo wa kufanya ngono mwezi mmoja kabla ya kuachiliwa kwa msamaha.

Hadi sasa kuna majimbo saba , mkiwemo Louisiana na Florida, yenye sheria ya kumaliza nguvu za kiume kwa wanaopatikana na hatia ya kuwabaka watoto wadogo.

Muswada wa sheria hiyo ulitiwa saini na Gavana wa jimbo la Alabama Kay Ivey Jumatatu. "Hii ni hatua kuelekea kuwalinda watoto katika jimbo la Alabama," Alisema Bi Ivey.

Hatua hiyo awali ilipendekezwa na Mbunge wa chama cha Republican, Steve Hurst. Alisema amekuwa akiathirika sana kwa kusikiliza ushahidi kutoka kwa mashirika yanayowalea watoto kuhusu namna watoto wadogo wanavyobakwa.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...