Search This Blog
Wednesday, June 26, 2019
Wanaodai biashara zinakufa, Serikali yawajibu
Serikali imesisitiza kuwa hali na mwenendo wa biashara nchini inakwenda vizuri, jambo linaloiwezesha kutekeleza miradi ya maendeleo, kulipa wafanyakazi mishahara, lakini pia kuwa na mazingira mazuri ya kuongeza idadi ya biashara zinazoanzishwa.
Aidha, imeendelea kuweka msimamo wake wa kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye taulo za kike isipokuwa inapunguza kodi ya Corporate Income Tax kutoka asilimia 30 hadi 25 kwa viwanda vinavyozalisha taulo hizo nchini kwa muda wa miaka miwili.
Hayo yamebainishwa kwa nyakati tofauti na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango na Naibu Waziri wake, Dk Ashatu Kijaji wakati wakijibu hoja za wabunge takribani 236 waliochangia katika mjadala wa kupitisha Bajeti ya Serikali Kuu kwa mwaka wa fedha 2019/20, bungeni.
Dk Kijaji amesema hali ya mwenendo wa biashara nchini ni nzuri na inazidi kuimarika tofauti na madai ya wabunge waliochangia huku wengine wakitumia takwimu zisizo sahihi kuhusu hoja kwamba hali ya biashara ni mbaya nchini.
Alisema alishawahi kueleza awali kuwa takwimu zinazowasilishwa bungeni humo kuwa biashara zinakufa nchini si sahihi na kuweka bayana takwimu halisi zinazoonesha kuwa biashara zinazofungwa ni 16,252 wakati zilizofunguliwa ni 147,817.
Alielezea sababu za biashara kufungwa ambazo zinawakabili wafanyabiashara dunia nzima kuwa ni mfanyabiashara kubadili biashara, kuzidiwa na ushindani kwa biashara husika, kushindwa kufanya biashara na mzigo mkubwa wa madeni ya kodi na benki.
"Zipo tafiti duniani zinazoonesha zaidi ya asilimia 50 ya biashara za kati na ndogo hufa kabla ya kusherehekea mwaka wa kwanza wa uanzishwaji wake, na hili si kwa Tanzania tu bali dunia nzima," alisema.
Alisema pamoja na ukweli huo, kupitia biashara zinazoendelea nchini serikali imekuwa ikiingiza mapato mengi na hivyo kutekeleza shughuli zake za kawaida ikiwemo kulipa mishahara kwa watumishi wake, lakini pia kuendeleza miradi ya maendeleo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment