Search This Blog
Thursday, June 27, 2019
Wachimba mgodi 36 wafariki DRC
Watu 36 wamefariki katika mgodi mmoja siku ya Alhamisi baada ya upande mmoja wa mgodi huo wa shaba kuporomoka kusini mashariki mwa Congo, kulingana na gavana wa mkoa huo.
Ajali hiyo ilitokea katika shimo la mgodi huo wa kampuni ya Kamoto Copper Company KCC , ambayo ni kampuni tanzu ya kampuni kubwa ya uchimbaji madini duniani Glencore yenye umiliki wa asilimia 75 ya hisa zake alisema Richard Muyej Gavana wa mkoa wa Lualaba.
''Ajali hiyo ilisababishwa na wachimbaji haramu waliovamia mgodi huo'', aliambia shirika la habari la Reuters, hatua hiyo ilifanya eneo moja la mgodi huo kuporomoka katika shimo hilo.
''KOV ni eneo linaloweza kuharibika kwa urahisi na ni hatari'', aliongeza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment