Kundi la waandamanaji linaloongozwa na taasisi ya wanataaluma nchini Sudan, hapo jana lilitangaza kampeni ya uasi wa kiraia wa nchi nzima hadi hapo utawala wa kijeshi utakapokabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia.
Kampeni hiyo iliyotangazwa kuanza rasmi leo, imeitishwa muda mfupi baada ya waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kuitembelea Sudan, kwa lengo la kufufua mazungumzo kati ya viongozi wa waandamanaji na baraza la mpito la kijeshi.
Hayo yanaendelea ikiwa ni masaa kadhaa tangu kukamatwa kwa baadhi ya viongozi wakuu wa upande wa upinzani ambao pia walihudhuria mazungumo na waziri mkuu wa Ethiopia. Sudan imekuwa katika hali ya sintofahamu tangu ulipoingia madarakani uongozi wa kijeshi, mara baada ya kung'olewa kwa aliyekuwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Omar Al Bashir.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment