Search This Blog
Monday, June 10, 2019
TCRA yatoa onyo kwa Wananchi usajili laini za simu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imewaonya wananchi kutosajili laini zao kwa mfumo mpya wa alama za vidole kwa kutumia maduka ya mtandaoni (Application), bali wahakikishe wanasajiliwa na mtoa huduma wa mawasiliano.
Imewataka pia kutumia fursa ya Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kupata huduma ya utatuzi wa matatizo yatokanayo na matumizi ya huduma za mawasiliano.
Ofisa Mwandamizi Masuala ya Mawasiliano na Uhusiano wa TCRA, Mabel Masasi ametoa onyo hilo wakati wa kampeni hiyo iliyofanyika kwenye viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Masasi alisema wananchi wanatakiwa kutosajili laini zao za simu kwa kutumia mifumo mingine bali wanatakiwa kufanya hiyo kupitia mtoa huduma.
Wananchi waende kusajili laini zao kwa mtoa huduma, ila niwasihi wananchi usitoe taarifa zako kwa mtu ambaye si mtoa huduma, wahalifu wamekuwa wakibuni njia mbalimbali za kupata taarifa binafsi za watu ili waweze kuzitumia vinginevyo.
"Sisi kama Mamlaka ya Mawasiliano jukumu letu ni kutoa elimu na tunawaelimisha watu kwamba msisajili laini zenu kwa kutumia Application (mfumo) ya aina yoyote, nenda kwa mtoa huduma ndiye atakayekusajilia na si vinginevyo."
Mkuu wa Kanda ya Kati wa TCRA, Antonio Manyanda alitoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanafanya usajili wa laini zao za simu kwa njia ya alama za vidole ili kujiepusha na usumbufu wa kufungiwa line zao ifikapo Desemba 31, mwaka huu.
"Baada ya muda huo kupita, laini ambazo hazitakuwa zimesajiliwa kwa njia hii zitakosa mawasiliano, tunafanya hivi kwa sababu usalama ni sehemu ya usajili huu, ukisajili kwa njia hii unakuwa salama na nchi inakuwa salama, hivyo wananchi wasiogope waje kusajili laini zao za simu maana lengo ni kuwaboreshea huduma za mawasiliano."
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, akitoa maelekezo kwa Kai...

No comments:
Post a Comment