Search This Blog
Monday, June 10, 2019
Mwadui FC kusuka kikosi kipya
Uongozi wa Mwadui FC umesema kuwa kwa sasa hesabu zao ni kusuka kikosi kipya kitakacholeta ushindani mkali msimu ujao baada ya kubaki kwenye Ligi Kuu Bara.
Katibu wa Mwadui, Ramadhan Kilao amesema kuwa baada ya kubaki kwenye ligi mpango wa kwanza ni kusuka kikosi upya.
"Tumenusurika kushuka daraja kutokana na kushindwa kumudu ushindani kwa msimu uliopita, kwa sasa tunaangalia namna bora itakayotufanya tuwe bora kwenye ushindani msimu ujao.
"Kikosi makini na chenye nguvu tutakuwa nacho msimu mpya hivyo mashabiki na wadau waendelee kutupa sapoti kama ambavyo walikuwa nasi bega kwa bega kwenye mchezo wetu wa playoff dhidi ya Geita," amesema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment