Search This Blog
Sunday, June 9, 2019
REA yakalia kooni wakandarasi wazembe
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Amos Maganga amesema hawatasita kumnyang'anya kazi mkandarasi atakayeshindwa kutekeleza mkataba wake ifi kapo Disemba mwaka huu.
Aidha, kunyang'anywa huko kutakwenda sambamba na kampuni hizo kulipa gharama ambazo zitatokana na ucheleweshwaji wa kuunganisha nishati ya umeme kwa wananchi.
Maganga aliyasema hayo baada ya kikao kilichoikutanisha Bodi ya REA na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza pamoja na kampuni zinazozalisha vifaa vinavyotumika kwenye mradi huo ambavyo ni transfoma, nguzo, nyaya na mita.
Alisema katika kikao hicho wamekubaliana Mradi wa REA Awamu ya Tatu mzunguko wa kwanza ukamilike Desemba mwaka huu ili miezi sita iliyobaki itumika kukamilisha matatizo madogo kwenye mradi.
"Mpango uliopo ni kuwa mradi huo ukamilike kati ya mwezi Mei na Julai mwakani, hadi Juni mwaka 2020, lakini katika kikao hiki tumekubaliana wakandarasi na wasambazajiwa wa vifaa wahakikishe mradi huu unakamilika Desemba ili miezi sita inayobaki 2020 iwe ni kazi ya kumaliza matatizo madogo madogo, hilo ndio tumeondoka nalo,alisema Maganga.
Aliongeza, "Kwanza wakandarasi wale ambao tunawaona hawafanyi vizuri tumeshakaa nao vikao na kwa bahati nzuri wengine wameanza kubadilika. Mkataba upo wazi kwamba wale wakandarasi watakaoona kwamba kufika Desemba hawataweza kumaliza mikataba yao ni kwamba serikali kupitia REA watakuwa tayari ku-terminate (kukatisha) mikataba yao na kuwanyang'anya kazi.
"Na sio hilo tu kwa sababu tukiwanyang’anya mikataba kuna consequence (madhara) watazipata moja, tutawaripoti kwenye vyombo vinavyohusika ili kampuni hizo zisipate kazi kabisa.
Lakini la pili kwa nini wamewa-delay (wachelewesha) Watanzania wasipate umeme kwa hiyo tutakuwa na hoja ya kusema hawa wamewa-delay Watanzania walikuwa wapate umeme ndani ya miezi hii, lakini sasa wanawafanya wapate umeme baada ya mwaka au miaka miwili mbele kwa hiyo kutakuwa na gharama tutawadai wafidie ile athari ambayo Watanzania wamepata kwa kukosa umeme na tukawanyang'anya ile mikataba.
Kwa hiyo wakandarasi wajipange sio suala tu la kuwanyanganya mikataba, lakini na consequence za kuwanyang'anya mikataba nalo litaambatana, alisema bosi huyo wa REA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...
No comments:
Post a Comment