Search This Blog
Tuesday, June 25, 2019
Rais Museveni akutana na Xi Jinping wa China
Rais Xi Jinping wa China amekutana na mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni ambaye yuko ziarani nchini China. Marais hao wawili wamekubaliana kuinua uhusiano kati ya nchi hizo mbili kuwa uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano wa pande zote.
Rais Xi Jinping amesema China inapenda kushirikiana na Uganda, kutumia fursa ya ujenzi wa 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' na utekelezaji wa matokeo ya mkutano wa kilele wa Beijing wa FOCAC, kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kuendelezwa zaidi na kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili.
Kwa upande wake rais Museveni, amesema Uganda inatumai kuzidisha ushirikiano wa pande mbili katika sekta mbalimbali, kwa kutumia fursa ya kujenga uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa pande zote kati ya nchi hizo mbili. Amesema vitendo vya upande mmoja ni hatari, Uganda na China zinapaswa kuimarisha mawasiliano na uratibu katika mambo yanayohusu pande nyingi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment