Search This Blog
Monday, June 24, 2019
Rais Magufuli azuru ujenzi wa Daraja la Baharini
John Magufuli hapo jana aliembelea mradi wa ujenzi wa daraja linalokatiza baharini kwa kuunganisha maeneo ya Aga Khan na Coco Beach Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujionea maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo.
Rais Magufuli ameshuhudia shughuli za ujenzi zikiendelea vizuri ambapo mkandarasi ambaye ni kampuni ya GS Engineering ya Korea anakamilisha kuunganisha daraja la muda litakalomwezesha kuanza ujenzi wa nguzo za daraja.
Akiwa katika Rais Magufuli amekutana na Mhandisi Mshauri kutoka kampuni ya Yooshin Engineering Mhandisi Suk-Joo Lee na kumuelezea kufurahishwa kwake na maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo ambalo linatarajiwa kusaidia kupunguza msongamano wa magari kutoka na kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Naye Suk-Joo Lee ameelezea kufurahishwa kwake kufanya kazi Tanzania na ameahidi kuwa kazi hiyo itakwenda vizuri.
Daraja hilo litakuwa na urefu wa kilometa 1.03 na barabara za kuunganisha zenye urefu wa kilometa 6.23 na utagharimu takribani shilingi Bilioni 255. Daraja hilo limependekezwa kuitwa Tanzanite Bridge na litarajiwa kukamilika mwezi Oktoba 2021.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment