Search This Blog
Monday, June 24, 2019
Polisi wamshikilia Baba anayetuhumiwa kumfanya vibaya mwanaye
Jeshi la Polisi mkoani Pwani linamshikilia Suleiman Issa Ngorombwe mfanyabiashara na mkazi wa Mailmoja Tangini, Kibaha kwa kudaiwa kumbaka na kumlawiti binti yake wa miaka 11.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa alieleza kwamba tuhuma hizo ziliripotiwa katika Kituo cha Polisi Kibaha Mjini, Juni 20 majira ya asubuhi ambapo walimkamata mtuhumiwa.
"Baada ya upelelezi wa tuhuma hii kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani," amesema.
Alieleza kuwa, jeshi la polisi linaendelea kukemea vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na vya kinyama vinavyofanywa na baadhi ya watu kwenye jamii.
Wankyo alisema, vitendo vya aina hiyo huanzia ngazi ya familia hivyo alitoa rai kwa wananchi kutoa ushirikiano wa kuripoti taarifa za matukio kama hayo ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria na iwe fundisho kwa wengine.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment