Pamoja na kuwa hana historia ya kucheza soka England wala hajawahi kuishi katika taifa hilo, Diego Maradona ameamua kuweka wazi hisia zake juu ya kuitamani ajira ya kocha wa sasa wa Man United Ole Gunnar Solskjaer na anaamini anaweza kuwa mbadala sahihi katika kiti hicho.
Maradona ambaye hana CV nzuri katika nafasi ya ukocha tofauti na kiwango chake enzi anacheza, ameeleza kuwa Man United ndio club pekee ya England ambayo amewahi kuiota kuifanyika kazi na anaomba kama watakuwa wanafikiria kutafuta kocha mwingine ni vyema wamfikirie yeye.
“Kama (United) wanahitaji kocha nafikiri mimi ni mtu sahihi wa kufanya kazi hiyo, Man United imekuwa ni club ya England ninayoipenda kwa muda mrefu sana lakini kwa sasa naweza kusema pia Man City, najua ni ngumu kubadili ila ni kwa sababu ya Aguero tunaongea sana na anacheza vizuri pale”>>> Diego Maradona
Historia ya Maradona katika nafasi ya ukocha haivutii sana licha ya baadhi ya vilabu kumuamini na kmpa nafasi, hadi sasa Maradona CV yake inaonesha amekaa katika vilabu kwa muda mchache hadumu sana, kwa sasa akiwa na club ya Dorados anahangahika kwa msimu wa pili kuipandisha Ligi Kuu timu ya ambayo inashiriki Ligi daraja la pili nchini Mexico kwa sasa.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment