Search This Blog

Sunday, June 9, 2019

Mambo mawilii yatakayojiri Ikulu leo


Rais John Magufuli leo atawaapisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa na Katibu Tawala Mkoa wa Njombe, Charles Kichere. Hatua hiyo inatokana na mabadiliko madogo aliyoyafanya, ambapo alitengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, & Kamishna Mkuu wa TRA.

Tukio hilo litafanyika Ikulu jijini Dar es Salaam kuanzia saa 8:00 mchana sanjari na kushuhudia tukio la makabidhiano ya fedha kutoka Airtel kwenda serikalini kiasi cha shilingi bilioni 5.27.

Miongoni mwa fedha zitakazotolewa, shilingi bilioni 2.27 ni kwaajili ya kuunga mkono juhudi za serikali katika maendeleo wakati shilingi bilioni TATU (3) ni malipo ya kila mwezi yatokanayo na umiliki wa hisa za Airtel Tanzania kati ya Serikali ya Tanzania na Bharti Airtel International.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...