Search This Blog
Thursday, June 27, 2019
Kauli ya Jaguar yatua ndani ya Bunge la EALA
Adan Mohamed ambaye ni Waziri wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Kanda wa Kenya ameliambia Bunge la Afrika Mashariki (Eala) kuwa nchi yake imejizatiti kikamilifu mwanachama mwaminifu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) licha ya matamshi yaliyotolewa na mbunge wa Starehe, Charles Njagua maarufu ‘Jaguar’.
Alitoa msimamo huo wa Serikali ya Kenya wakati wa kikao cha Bunge kuwa matamshi yaliyotolewa na mbunge huyo yamekera viongozi katika nchi yake pamoja na viongozi wengine kwenye kanda nzima ya EAC.
Waziri Mohamed alinukuu maneno ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa aliyoyatoa bungeni Juni 25, 2019 kuwa nchi zote zimedhamiria kuwa katika jumuiya hiyo ya kikanda na wanachama wake wasikubali kauli zenye kupanda mbegu za chuki kwa sababu wao ndugu katika jumuiya hiyo.
“Napenda kurejea msimamo wa Serikali ya Kenya kuwa msimamo wetu hautikisiki kuhusu mtangamano wa Jumuiya yetu, mkataba ulioanzisha EAC na itifaki zake ambayo tumeiridhia bado itaendelea kuiheshimu ikianzia na Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta,” alisema
“Mheshimiwa Spika na Bunge zima kama mnavyo fahamu, Rais Uhuru Kenyatta mara kwa mara amekua akizungumza hadharani akiwakaribisha wananchi wa Afrika Mashariki kwenda kuwekeza, kutembelea vivutio vyetu na hata kuoa na kuolewa na kuweka makazi yao huko ili mradi wanafanya hivyo kwa kuzingatia sheria,” alisema Mohamed.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment