Search This Blog

Sunday, June 23, 2019

Baada ya Harmonize, Vanessa Mdee naye kufanya yake


Msanii nyota wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee anajiandaa kuachia E.P yake (nyimbo chache zinazounganishwa pamoja) ambayo ameiita Expensive.

Katika uthibitisho wa hilo, ametuonesha Cover art ya EP hiyo ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni. Habari njema ni kwamba ndani ya EP hiyo pia Vanessa  ana Collabo na mdogo wake Mimi Mars.

Tayari Mimi Mars alithibitisha ujio wa Collabo hiyo akiwa kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio hapa nchini mwezi mei mwaka huu na pia alisema Collabo hiyo ndiyo iliyobeba jina la EP hiyo.

Vanessa Mdee atakuwa msanii wa pili kutoka kwenye Bongo Fleva kwa mwaka huu kuachia EP baada ya Harmonize aliyeachia ya kwake inayokwenda kwa jina la Afro Bongo.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...