Search This Blog
Friday, May 24, 2019
Waziri Mkuu Uingereza kujiuzulu Juni 7
Theresa May kujiuzulu kama kiongozi wa chama cha Conservative Juni 7 na kutoa fursa kuidhinishwa mchakato wa kuchaguliwa waziri mkuu mpya Uingereza.
Katika taarifa iliyojaa hisia aliyoitoa huko Downing Street, Bi May amesema amefanya "kila awezalo" kutekeleza matokeo ya kura ya maoni kuhusu EU ya mnamo 2016.
Ni jambo linalosalia kuwa "na majuto mengi" kwamba ameshindwa kutimiza Brexit - Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, ameongeza.
Lakini waziri mkuu mpya ndio suluhu " kwa manufaa ya taifa".
Bi May amesema ataendelea kuhudumu kama waziri mkuu wakati kukitarajiwa kuidhinishwa mchakato wa kumchagua kiongozi mpya wa chama cha Conservative.
Atajiuzulu kama kiongozi wa chama hicho Juni 7 na uteuzi wa waziri mkuu mpya unatarajiwa kuanza wiki inayoafuata baada ya hatua hiyo.
http://bit.ly/2Ew9rCj
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment