Search This Blog

Thursday, May 23, 2019

Waziri Kalemani awataka wananchi kutunza miundo mbinu ya Umeme


Na Amiri kilagalila,

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amewataka wananchi kutunza miundombinu ya Umeme inayopita katika Vijiji vyao.

Akizungumza katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Masasi Jana, Waziri Kalemani amesema kuwa Serikali inatumia gharama kubwa kufikisha Umeme na kuwataka wananchi wasifanye shughuli zitakazo athiri miundombinu ya Umeme ikiwemo kuwasha moto karibu na Nguzo na badala yake wahamasike kulipia huduma hiyo ili iweze kuwasaidia katika shughuli zao za kiuchumi.

Akiwasha umeme katika Vijiji vya Nanditi na Mombaka katika Wilaya ya Masasi Waziri amezitaka Halmashauri za Wilaya, kulipia gharama za Umeme za taasisi mbalimbali za kijamii ikiwemo Shule na zahanati na kudai umeme mara tu baada ya kulipia.

“Kabla ya kulalamika Shule haina umeme na Zahanati haina umeme, jiulize swali moja  tu umelipia?lipia kwanza ndo udai umeme, halmashauri zote za wilaya lipieni taasisi za umma, tunataka wananchi wapate umeme, na umeme pia ufike mashuleni, zahanati, na sehemu zote zinazotoa huduma” alisema Dkt. Kalemani  na kumtaka Mkandarasi kukamilisha  kuunganisha umeme katika vijiji 122vilivyobaki  katika kata ya Mndibwa, ndani ya siku 25.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Mhe. Selemani Mzee ameishukuru Serikali kwa kufikisha Umeme Masasi na kuwataka wananchi wote wa masasi kulipia Umeme.




http://bit.ly/2Wote0J

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...