Search This Blog

Thursday, May 23, 2019

Wakina mama watakiwa kuwa na muamko wa kuwapeleka watoto kupatiwa dawa za minyoo


Na Thabit Hamidu, Zanzibar.

Afisa Lishe kutoka Katika Kitengo cha Lishe Zanzibar Subira Bakari amewataka wakina mama ndani ya Mkoa wa Kaskazin B Unguja kuwa na muamko wa kuwapapeleka watoto wao kupatiwa dawa za Minyoo na vitamin A.

Wito huo aliutoa wakati akizungumza na waandishi wa habari na wadau mbalimbali wa Afya katika Ukumbi wa Hospitali ya wagonjwa wa akili kidongo Chekundu Mjini Unguja.

Alisema tafiti iliyofanywa mwezi Decemba mwaka jana inaonyesha kuwa Mkoa huo upo nyuma katika kuwapaleka watoto kupatiwa dawa za minyoo na Vitamini A.

Alieleza kutokana na Takwimu hizo jitihada mbalimbali zinahitajika katika kuwashajihisha wakinamama hao kuwapeleka watoto wao kupatiwa dawa hizo ili kuepukana na maradhi mbalimbali.

“Juhudi zinahitajika ili kukubaliana na tatizo hili ambapo wakina mama, wazazi na walezi kushindwa kuwapeleka watoto wao kupatiwa dawa”Alisema Afisa huyo.

Alifahamisha kuwa hali hiyo inatokana na sababu mbali mbali ikiwemo uelewa mdogo wa elimu ya afya na ushirikiano hafifu wanaoupata kutoka kwa Wadau tofauti wa Wilaya hiyo.

Hivyo alisema ipo haja kufanyika kwa mjadala wa pamoja kubaini chanzo cha tatizo ili kuifanya Wilaya hiyo kufikia viwango sawa na Wilaya nyingine.

Kwa upande wao washiriki wa Mkutano huo walipendekeza kutengenezwe Bajeti maalum ya kuongeza elimu ya Afya kwa Wilaya hiyo.

Aidha wamesema ipo haja ya kuishirikisha jamii yote ikiwemo Wazee na Walimu wa Madrsa badala ya kuwaachia Masheha na Wajumbe wao kusimamia zoezi la kuhamasisha jamii kutekeleza zoezi hilo.



http://bit.ly/2M13683

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...