Search This Blog
Thursday, May 23, 2019
Wanaoishi nje ya nchi kupiga kura 2020? Jibu hili hapa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali inaangalia uwezekano wa watanzania wanaoishi nje ya nchi kuweza kupiga kura katika uchaguzi ujao.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati akijibu maswali ya papo kwa papo bungeni ambapo alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Asha Abdalah Juma (CCM).
Katika swali lake Mbunge huyo ametaka kujua serikali ina mpango gani wa kuwashirikisha watanzania wanaoishi nje kupiga kura katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
“Ilani ya Chama cha CCM imetekelezwa kwa kiasi kikubwa pamoja na mambo mazuri je serikali ina mpango gani wa kuwawezesha watanzania wanaoishi nje waweze kupiga kura mwaka 2020” amehoji
Akijibu swali hilo Majaliwa amesema suala hilo ni la kisera na kwa sasa serikali inalifanyia kazi kuona jinsi gani watanzania hao wataweza kupiga kura.
Amesema ni lazima kwanza kujua idadi ya watanzania hao waliopo nje na wanafanya nini
“Hili ni jambo la kisera lakini kwanza tujue idadi yao na wapo wapi na wanafanya nini kabla ya kuruhusu kupiga kura” amesema
http://bit.ly/2WlVNMf
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment