Search This Blog

Monday, May 27, 2019

Wafungwa 15 wafariki kwenye vurugu zilizotokea gerezani


Kwa mujibu wa Sekretarieti ya Magereza, Wafungwa hao wamefariki jana Mei 26 katika gereza moja lililopo kwenye jimbo la Amazonas baada ya vurugu kuzuka.

Mkuu wa Sekretarieti hiyo, Kanali Marcos Vinicius Almeifa amesema, Wafungwa hao walifariki ama kwa kukosa hewa au kuchomwa na vitu vya ncha kali ikiwemo miswaki.

Ameeleza kuwa vurugu zilianza muda wa raia kutembelea Wafungwa, hakukuwa na raia waliotekwa nyara na vurugu hizo zilikuwa baina ya Wafungwa wenyewe.

Ameongezea kuwa bado sababu ya vurugu hizo haijafahamika ila Serikali inafanya uchunguzi kubaini chanzo hicho.

Aidha, mwaka 2017 katika gereza hilo hilo kulitokea vurugu zilizodumu kwa saa 20 ambapo Wafungwa walikuwa wakitaka kufanya mapinduzi na kupelekea watu 56 kufariki.

http://bit.ly/2K7b6Su

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...