Mkurugenzi wa Jiji la Arusha ,Dkt Maulid Madeni ameamuru kukamatwa na kuwekwa mahabusu mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko kuu jijini Arusha,Fredy Elphasi kwa kosa la kujimilikisha vibanda kinyume na utaratibu na kuvikodisha kwa wafanyabiashara wenzake bila makubaliano na halmashauri hiyo.
Akiongea ofisini kwake,Dkta Madeni amedai kuwa mwenyekiti huyo, Elphasi amekuwa akiendesha biashara ya kujenga vibanda bila idhini ya halmashauri hiyo na kisha kuvikodisha kwa wafanyabiashara wenzake kwa kiwango cha juu huku akiilipa halmashauri hiyo kiasi kidogo cha fedha jambo linaloisababishia hasara halmashauri hiyo.
TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE

No comments:
Post a Comment