Search This Blog

Thursday, May 30, 2019

PSSSF yatumia Bil. 880 kulipa Mafao


Wanachama elfu kumi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wamelipwa takribani Bilioni 880 ikiwa ni malimbikizo ya pensheni kwa wastaafu  tangu kuanzishwa kwa mfuko huo mapema mwaka jana.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma Meneja Kiongozi, Uhusiano  wa mfuko huo Bi. Eunice Chiume amesema kuwa dhamira ya  Mfuko huo ni kuhakikisha kuwa wanachama wake wanaendelea kulipwa mafao yao kwa wakati kuendana na azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kuwafanya wastaafu wote kuishi maisha bora.

“Katika kipindi cha miezi 6 Mfuko umeendelea kutoa huduma bora hali iliyowezesha wastaafu wetu zaidi124,000 kuendelea kupata huduma zetu katika ofisi zetu za mikoani pamoja na Zanzibar” alisisitiza Chiume.

Akifafanua amesema kuwa mfuko huo una wanachama takribani 763,000 kote nchini na unaendelea kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma bora kwa wanachama wake.

Mfuko huo umeendelea kutekeleza dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda kwa kusimamia uwekezaji katika sekta hiyo ikiwemo kiwanda cha viatu Karanga kilichopo Moshi  Mkoani Kilimanjaro kinachomilikiwa kwa ubia na Jeshi la  Magereza.
Eneo jingine ni uwekezaji katika amana za Serikali, kiwanda cha Tangawizi kilichopo Same Mkoani Kilimanjaro.

Kwa upande wa zoezi la uhakiki wa wanachama wa mfuko huo amesema kuwa zoezi hilo limefanyika kati ya Desemba 2018 hadi Machi 2019 na ni endelevu.

Mfuko wa PSSSF ni matokeo ya kuunganishwa kwa mifuko ya PSPF, LAPF, GEPF na PPF ili kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi hasa kuchochea ukuaji wa sekta ya hifadhi ya Jamii hapa nchini.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...