Search This Blog
Wednesday, May 29, 2019
Upinzani Sudan waandaa mgomo
Muungano wa upinzani nchini Sudan pamoja na makundi ya waandamanaji, wameshiriki mgomo kulishinikiza baraza la jeshi kuachia madaraka utawala wa kiraia.
Wahudumu wa afya, umeme na wafanyakazi wa benki walishiriki mgomo huo na katika sekta nyingine shughuli ziliathiriwa kidogo.
Kufuatia mgomo huo, baadhi ya mashirika ya ndege yalisitisha safari zao kutoka uwanja wa ndege wa Khartoum.
Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa mamia ya wasafiri walikwama katika uwanja wa ndege mjini Khartoum na katika baadhi ya vituo vya mabasi.
Kama hatua ya kuongeza shinikizo dhidi ya baraza la kijeshi linaloshikilia madaraka kwa sasa, vuguvugu linaloendesha maandamano kwa jina Freedom and Change, limeitisha mgomo wa kitaifa wa siku mbili kuanzia leo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment