Search This Blog

Wednesday, May 29, 2019

DC Ndejembi akagua hali ya vitambulisho vya wajasiriamali


Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe Deo Ndejembi amefanya ziara katika mnada wa Mkutani wilayani humo kukagua hali ya vitambulisho vya wajasiriamali ambavyo vilitolewa na Mhe Rais Magufuli.

Katika ziara hiyo DC Ndejembi aligawa vitambulisho 54 kwa wajasiriamali hao ambao walimshukuru Rais Magufuli kwa kuwaletea vitambulisho hivyo ambavyo vinawawezesha kufanya biashara sehemu yoyote nchini.

" Leo nimefika katika mnada huu wa Mkutani kukagua vitambulisho hivi, ambapo tumeweza kuwapatia wajasiriamali 54 papo kwa hapo leo na wajasiriamali wanashukuru sana uwepo wa vitambulisho hivi kwa Mhe Rais Magufuli kuwapa, kwa sababu kila mnada wanapokwenda wanatozwa Sh 500 lakini kwa hivi vitambulisho hawatochajiwa na wanafanya biashara nchi nzima," amesema DC Ndejembi.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...