Search This Blog
Monday, May 27, 2019
Trump kukutana na Mfalme mpya wa Japan Naruhito
Rais Donald Trump na mke wake Melania leo wamekutana na Mfalme mpya wa Japan Naruhito pamoja na Malkia Masako.
Trump aliyewasili nchini Japan siku ya Jumamosi kwa ziara ya siku nne, amekua mgeni wa kwanza wa kitaifa kukutana na Mfalme huyo tangu alipotawazwa mnamo Mei mosi, baada ya baba yake Akihito kutangaza kuachia madaraka.
Trump atafanya mazungumzo na waziri mkuu Shinzo Abe, ambayo yanatarajiwa kugubikwa na ajenda za biashara na Korea Kaskazini.
Trump ameishutumu mara kwa mara Japan kwa ziada ya biashara na Marekani na kutishia kuongeza ushuru kwa magari ya Japan pamoja na vifaa.
Lakini hapo jana alidai kuwepo na maendeleo mazuri katika mazungumzo ya kibiashara na Japan. Viongozi hao wawili jana walicheza Gofu na kutizama mchezo wa Zumo.
http://bit.ly/2W3SGJK
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment