Search This Blog
Thursday, May 23, 2019
RC Ayoub awataka wadau wa maendeleo kuwasaidia Vijana wenye mahitaji maalum
Na Thabit Hamidu, Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud amewataka Viongozi na wadau mbali mbali wa maendeleo Nchini kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuwasaidia vijana wenye mahitaji Maalum hususani katika suala zima la Kiimani.
RC Ayoub alisema kuwa hatua hiyo itasaiddia kujenga jamii iliyokuwa bora na yenye Imani ya kusaidiana kwa kila jambo.
Kauli hiyo ameitoa leo katika Bandari ya Malindi wakati wa Mapokezi Maalumu ya Kijina Shamsudeen Hussein Ali (22) alieshika nafasi ya Tatu katika mashindano ya Quran yaliyofanyika hivi karibu Jijini Dar es Salaam.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa viongozi mbalimbali katika jamii na wadau wa maendeleo hawana budi katika kusaidia vijana wenye mahitaji maalum hususani katika masuala ya kiimani ili jamii kujenga jamii iliyobora na yenye kusadiana kwa hali na mali.
“Tukiwa watu wa kusaidiana na kuendelezana tutajenga jamii yenye ustawi mzuri na tutapata barka kwa kila jambo tunaloliendea” alieleza Ayoub.
Aliongeza kuwa ushindi wa Hasnudin katika mashindano hayo ni faraja kwa Zanzibar na kuthibitisha juhudi zinazochukuliwa na taasisi mbali mbali za kidini na serikali katika kuendeleza mbele dini ya kiislamu.
Aidha alisema walimu hao wanafanya kazi kubwa katika kuwajenga kimaadili, kuwaongezea ujuzi na maarifa vijana kwa kuhifadhi kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu ambacho ni muongozo kwa wanadamu na wauini wa dini ya kiislam.
Hata hivyo alimpongeza mshindi huyo kwa kuiletea sifa Zanzibar na Tanzania kwa ushindi wake na kuahidi kumpatia fedha taslim shilingi milioni moja na kompyuta mpakato (laptop) kama nyongeza ya zawadi ili kuibua ari ya vijana wengine kujifunza na kukihifadhi kitabu hicho.
http://bit.ly/2M4F5gq
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment