Search This Blog
Tuesday, May 28, 2019
RC akemea baadhi ya Madiwani wanaoingiza siasa kwenye shughuli za wataalamu
Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Mhandisi Evarist Ndikilo amekemea baadhi ya madiwani kuacha kuingiza siasa kwenye shughuli za wataalamu katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa hospital za wilaya unaoendelea kujengwa kwenye halmashauri tatu za mkoa huo.
Aidha amezitaka, halmashauri zinazojengwa hospital hizo ikiwemo Kibaha Mji,Kibiti na halmashauri ya wilaya ya Kibaha kuhakikisha wanamaliza ujenzi huo ifikapo juni 25 mwaka huu.
Akizungumza wakati alipotembelea ujenzi unaondelea katika halmashauri za wilaya ya Kibaha,Ndikilo aliwataka baadhi ya wanasiasa na watendaji kukwamisha kwa namna yoyote miradi ya kitaifa na kimkoa kwa maslahi ya matumbo yao.
Alisema ,katika kukabiliana na changamoto ya utoaji wa huduma ya afya kwa jamii serikali ya awamu ya tano inajenga hospitali za wilaya tatu za kisasa ,mkoani hapo ambazo zitagharimu kiasi cha sh. bilioni 4.5.
Ndikilo alielekeza, fedha zote zinazoelekezwa katika miradi hiyo muhimu zitumike kwa wakati na kwa matumizi lengwa bila kuziacha kubaki viporo.
“Uzoefu tulioupata kwamba kwanini tunachelewa chelewa sana ni baadhi yetu kutaka fedha hizi ,hii hii bilioni 1.5 kwa kila halmashauri wanajiwekea nipate asilimia 10, fundi wangu ,mjomba wangu apate tenda ya ufundi ,ndugu yangu alete matofali na kutusababishia kuchelewa malengo yetu,”alifafanua Ndikilo.
Nae mkuu wa wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama alieleza changamoto kubwa iliyosababisha kuchelewa kidogo kwa ujenzi ni hali ya mvua hivyo wanaomba kuongezwa muda japo siku 20 badala ya juni 25 mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment