Search This Blog

Tuesday, May 28, 2019

Kansela wa Austria aondolewa madarakani


Wabunge wa Austria leo wameiondoa madarakani Serikali ya Kansela Sebastian Kurz baada ya kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.

Kura hiyo dhidi ya kiongozi wa nchi na serikali au baraza lake la Mawaziri ni ya kihistoria nchini Austria tangu kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Kura hiyo imeungwa mkono na wabunge kutoka Chama cha Social Democrats na Chama cha Freedom kinachofuata siasa kali za mrengo wa kulia, ambacho kilikuwa katika serikali ya muungano ya Kurz hadi wiki moja iliyopita ambapo kiongozi wake alijiuzulu kutokana na kashfa ya rushwa.

Kwa mujibu wa katiba Rais wa Austria, Alexander Van der Bellen sasa anapaswa kumteua kansela mpya ambaye ataunda serikali ambayo itaungwa na mkono na bunge hadi uchaguzi mkuu utakapofanyika, Uchaguzi unatarajiwa kufanyika mwezi Septemba.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...