Search This Blog
Thursday, May 30, 2019
Raia wa Ufaransa ahukumiwa kifo Iraq kwa kujiunga na IS
Mahakama ya mjini Baghdad nchini Iraq imemhukumu kifo raia mmoja wa Ufaransa leo kwa kujiunga na kundi la itikadi kali linalojiita dola la kiisalamu.
Hatua hiyo imeifanya idadi ya wapiganaji wa jihadi ambao ni raia wa ufaransa wanaokabiliwa na hukumu ya kifo kuwa saba.
Yassin Sakkam alikuwa miongoni mwa raia 12 wa Ufaransa waliokabidhiwa kwa mamlaka za Iraqi mwezi Januari na vikosi vya Marekani vinavyopambana na kundi hilo la kigaidi nchini Syria.
Sakkam amekiri mbele ya mahakama kula kiapo cha kulitumikia kundi la IS akisema alikuwa akipokea kila mwezi dola 70.
Sakkam ambae ana umri wa miaka 29 amesema mahakamani kwamba anajutia uamuzi wake wa kujiunga na kundi hilo na ameomba kusamehewa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment