Search This Blog

Tuesday, May 28, 2019

Pesa yako, simu yako, ni hatari kwa Afya yako



Watafiti wameonya kuhusu athari za kiafya zinazoweza kupatikana kutokana na matumizi ya simu na fedha chafu.

Fedha, haswa ya sarafu, wanasayansi wanasema kwamba vimelea vya magonjwa kama ya kuhara na magonjwa mengine mengi ambayo yanaweza kupatikana katika katika chakula ni rahisi mtu kupata.

Utafiti huo ambao ulifanywa kwa wauza chakula wapatao 395 katika maeneo tofauti tofauti ya jiji la Nairobi, nchini Kenya na wataalamu kutoka chuo cha Kilimo na teknolojia, Taasisi ya utafiti wa dawa na watafiti kutoka Marekani, umeonyesha kuwa vimelea vinavyopatikana katika simu pamoja na fedha hutengeneza sumu katika chakula

Walifanya uchunguzi wa sarafu ambazo zinazunguka sana ndani ya Nairobi na ripoti ilibaini kuwa shilingi 5, 10 na 20 ndio zilikuwa chafu zaidi ikifuatiwa na shilingi 50, 100 na 200.Pesa nyingi ambazo zinazunguka sana na simu zilikutwa na vimelea vidogo vinavyoambukiza magonjwa.

Jambo baya zaidi katika migahawa au maeneo yanayouza chakula, haswa wahudumu na wapishi kutokuzingatia usafi baada ya kutumia simu zao.Wakati wa utafiti, washiriki 34 walikutwa wagonjwa huku wengine wakiwa wanasumbuliwa na kikohozi, magonjwa ya tumbo na homa.

Magonjwa haya yalikuwa hayawasumbui wagonjwa peke yake, lakini pia yalikuwa yanasambaa katika chakula ambacho mhudumu wa chakula au mpishi alikuwa anakiandaa.Hata hivyo, zaidi ya asilimia 60 walikuwa hawajaosha mikono yao baada ya kushika pesa au kutumia simu.

Kwa mujibu wa mtafiti Dkt.Richard Korir kutoka kituo cha utafiti cha Kemri, amesema kuwa vimelea hivyo vya magonjwa vinaenea kwa haraka kwa sababu watu hawasafishi mikono yao na kutozingatia usafi wa mazingira yanayowazunguka na hivyo kusababisha bakteria kuenea katika chakula.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...