Search This Blog
Monday, May 27, 2019
Nina imani na kiongozi wa Korea Kaskazini - Rais Trump
Rais Donald Trump wa Marekani amesema kuwa ana imani na kiongozi wa Korea Kaskazini licha ya majaribio ya silaha yaliyofanywa hivi karibuni pamoja na kukwama kwa mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia.
Trump ambaye yuko Japan kwa ziara inayolenga kuimarisha mahusiano na mshirika huyo muhimu wa Marekani, amesema hivi leo kuwa majaribio ya silaha nchini Korea Kaskazini yaliyofanywa mapema mwezi Mei siyo jambo linalomtia wasiwasi. Matamshi ya Trump yanatofautiana na ya mshauri wake wa masuala ya usalama, John Bolton, ambaye hapo jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa Korea Kaskazini imekiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa kwa kufanya majaribio ya silaha.
Lakini katika ukarasa wake wa Twitter, Rais Trump ameandika kuwa ana matumaini Kim Jong Un ataheshimu ahadi aliyoitoa kuhusu suala la majaribio ya silaha. Korea Kaskazini ni moja ya masuala muhimu ya majadiliano wakati Trump atakapokutana na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe.
http://bit.ly/2HVLlSp
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment