Search This Blog

Wednesday, May 29, 2019

Naibu spika aichangia Klabu ya Yanga


Naibu  Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson ametoa Sh. milioni moja kwa ajili ya kuichangia Klabu ya mpira wa miguu ya Yanga huku akitoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa kuichangia timu hiyo.

Dk Tulia ametoa mchango huo leo, Ofisini kwake bungeni jijini Dodoma kwa kuukabidhi kwa viongozi ambao ni wabunge wapenzi wa Yanga wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya kuhamasisha michango ya timu hiyo, Anthony Mavunde.

Wabunge wengine waliokuwepo katika kupokea mchango huo ambao ni wapenzi wa Yanga ni Hawa Ghasia (Mtwara Vijijini-CCM), Vanance Mwamoto (Kilolo-CCM), Mohamed Mchengerwa (Rufiji-CCM) na Mussa Ntimizi (Igalula-CCM).

Akizungumza kabla ya kukabidhi mchango huo, Dk.Tulia  amesema aliahidi kuichangia timu hiyo na sasa anatimiza ahadi yake.

“Niliahidi kuchangia Yanga na nimekabidhi Sh. milioni  moja na ninawaomba sana Watanzania kuwachangia Yanga kwani wanahitaji sana michango.”amesema Dk Tulia.

Aidha ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza Juni 15, 2019 katika shughuli iliyoandaliwa na Yanga ambayo imepewa jina la ‘Kubwa Kuliko’ itakayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...