Search This Blog
Monday, May 27, 2019
Mwalimu wa Madrasa ahukumiwa maisha kwa kumbaka mwanafunzi wa miaka tisa
Mwalimu wa Madrasa mkazi wa Unyankindi manispaa ya Singida, Bw.Daudi Idd Karata mwenye umri wa miaka sabini na sita,amehukumiwa na mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida ,adhabu ya kutumikia jela maisha yake yote yaliyobaki, baada ya kupatikana na hatia ya kubaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka tisa.
Mwanafunzi huyo jina limehifadhiwa akati akibakwa,alikuwa akisoma darasa la pili katika shule ya msingi Unyankindi mjini Singida ambapo mshitakiwa huyo ambaye pia ni mfanyabishara na mganga wa kienyeji,alikuwa akiishi karibu na shule ya msingi Unyankindi.
Mshitakiwa Karata, pamoja na kuhukumiwa kutumika jela maisha yake yote bado anakabiliwa na kesi nyingine ya ubakaji inaendelea katika mahakama hiyo ambayo imeanza kusikilizwa kuanzia Oktoba 23 mwaka 2017.
katika kesi hiyo,mshitakiwa anatuhumiwa kubaka wanafunzi 14 kutoka shule za msingi Singidani,Nyerere na Mughanga huku wanafunzi hao mwenye umri kati ya miaka saba na kumi na mbili,walikuwa wakirubuniwa kwa kupewa zawadi ya pipi,kuangalia tv,shilingi 200,au shilingi 2,000.
http://bit.ly/2JJ1ez5
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment