Search This Blog

Friday, May 31, 2019

Mrembo Poshy Qeen Silazimishi Sanchi Kunifahamu


Mrembo ambaye jina lake limekuwa kubwa mjini kutokana na umbo lake tata, Jacqueline Obeid ‘Poshy’ amemfungukia mrembo mwenzake, Jane Rimoy ‘Sanchi’ na kusema hamlazimishi kumfahamu. Akizungumza na Ijumaa, Poshy alisema kuwa kama mtu hamjui ni kawaida na pia hamlazimishi amjue kwa sababu hata kama atamjua itakuwa haina faida yoyote au hasara kwake.

“Kama mtu hakujui huwezi kumlazimisha akujue hata siku moja ni ngumu kwanza hivyo yeye anijue asinijue naona sawa tu mimi,” alisema Poshy. 

Poshy amefunguka hayo baada Sanchi kusema kuwa hamfahamu wala hajawahi kumsikia alipokuwa akihojiwa na chombo kimoja cha habari hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...