Search This Blog
Sunday, May 26, 2019
Kinyang'anyiro cha kumrithi Theresa May kuanza leo
Wagombea wanaowania kumrithi Theresa May kama waziri mkuu wa Uingereza wanajiandaa kuanza kampeni zao hii leo, na kuacha mchakato wa kujiondoa Umoja wa Ulaya-Brexit ukiwa mashakani.
May alitangaza kujiuzulu wadhifa wake jana Ijumaa na kusababisha kuanza kwa kinyang'anyiro cha kumsaka mrithi wake ndani ya kipindi cha miezi miwili. May atajiuzulu kama kiongozi wa chama cha Conservative mnamo Juni 7 lakini atasalia kama waziri mkuu hadi pale chama kitakapomchagua mrithi wake kufikia Juni 20.
Tarehe ya Uingereza kuondoka Umoja wa Ulaya imepangwa Oktoba 31 ingawa kiongozi yeyote mpya anaweza kuomba mchakato kucheleweshwa.
Waziri wa zamani wa mambo ya nje Boris Johnson ni miongoni mwa waliotangaza nia sambamba na waziri wa zamani wa Brexit Dominic Raab. Kiongozi wa upinzani Jeremy Corbyn amesema yeyote yule atakayechaguliwa atapaswa kuitisha haraka uchaguzi mkuu.
http://bit.ly/2wkzQi1
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment