Search This Blog
Thursday, May 30, 2019
Iran yakanusha vikali madai ya Marekani kuhusu kushambulia Meli
Iran imepinga vikali madai yaliyotolewa na mshauri wa masuala ya usalama wa taifa wa Marekani John Bolton leo kwamba kwa kiasi kikubwa inauhakika mashambulizi ya Mei 12 dhidi ya meli nne katika bandari ya Emarati yalifanywa na Iran.
Bolton alitowa kauli hiyo leo akiwa ziarani Emarati, Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje wa Iran Abbas Moussavi ametowa taarifa kupitia tovuti rasmi ya Wizara hiyo akisema Marekani kutowa madai kama hayo ya kuchekesha sio jambo la kushangaza.
Mvutano kati ya Marekani na Iran umeongezeka tangu Rais wa Iran Hassan Rowhani kutangaza mwanzoni mwa mwezi huu kwamba nchi yake itaanza hatua kwa hatua kujiondowa katika makubaliano ya Nuklia ya Mwaka 2015 iliyoyafikia na nchi zenye nguvu duniani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...

No comments:
Post a Comment