Search This Blog

Thursday, May 30, 2019

RC Makonda kuwasaka wasiona vitambulisho vya ujasiliamali


Mkuu waMkoa  wa  Dar es salaam, Paul Makonda ametangaza msako kwa wafanyabiashara wadogo wasiokuwa na vitambulisho vya ujasiliamali vilivyo anza kutolewa mapema mwanzoni mwa mwaka  huu.

Msako huo ni moja ya mkakati wa ukusanyaji mapato kupitia wafanyabiashara hao.

Paul Makonda amesema Juni 3 mwaka huu ni marufuku kwa mfanyabiashara yoyote mdogo kujishughulisha na biashara ndani ya mkoa huo bila kuwa na kitambulisho maalumu cha utambuzi kilichotolewa na Rais Dk John Magufuli.

Sambamba na hilo,mkuu wa mkoa huyo amewasihi wafanyabiashara hao walipe kodi ili waongeze wastani wa pato la taifa kupitia kodi.

Aidha Makonda amewataka wafanyabiashara wasiopata vitambulisho lakini wanavigezo vya kuvipata wafike sehemu husika ikiwemo ofisi za wakuu wa mikoa ili kuvipata.

Amesema takwimu kubwa zinaonyesha kuwa idadi ya wafanyabiashara wasiokuwa na vitambulisho ni kubwa.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...