Search This Blog
Thursday, May 30, 2019
Mbunge ataka REA iunde tume maalum kusimamia miradi ya umeme
Mbunge wa Viti Maalumu, Upendo Peneza (CHADEMA), ameitaka Wizara ya Nishati kuunda kitengo maalumu cha kusimamia miradi ya umeme ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA).
Kauli hiyo ameitoa leo, bungeni jijini Dodoma, wakati akichangia mjadala wa Wizara ya Nishati kwa mwaka 2019/20 ambapo amesema kumekuwa na changamoto katika usimamizi wa miradi ya Rea.
“Mradi wa Rea mnachelewesha fedha hatimaye inazalisha ongezeko la fedha kwa wasimamizi wa miradi, hata wale wanaofanya hizo kazi wapo wanaochelewesha.
“Naiomba Wizara iunde kitengo maalumu kwa ajili ya kushughulikia miradi yote ya Rea kuepusha changamoto hizo,” amesema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...

No comments:
Post a Comment